 |
Jengo la waandishi wa habari
Jengo la waandishi wa habari ni mahali ambapo huwapokea waandishi wa habari wanao hama nchini kwao kutokana na matatizo mbalimbali na kuwapa mahali pa mapumziko yaani waandishi hao wa habari hupewa malazi na pia mazoezi kwa shuhuli yao.
Miongoni mwao (waandishi wa habari, watangazaji, wapiga picha, ma ripota na kadhalika...) ambao tunao patia malazi hakuna ambae alie pendelea kwa hiyari yake mwenyewe kuihama nchi yake .
Kinacho muakilisha mwanadamu ni mapenzi,watoto,marafiki,majirani,malazi pia ardhi.
Mkimbizi huyo alilazimishwa kwa kujisalimisha asalie hivyo vitu vyote. Hofu na mashaka ni kwa familia yake inayo baki nyuma. Mwandishi wa habari yeyote huwakilishwa na shuhuli yake, yeye hutoa habari, hufanya uchunguzi, hutoa ripoti, hayo yote kwa manufaa ya raiya ambao hustahili kufahamu na kuelewa vyema habari mbalimbali.
Mwandishi huyo wa habari ambae yuko uwamishini hujihisi kua hafai anapofika katika nchi hiyo inayo mpa hifadhi. Katika jengo hilo la wandishi wa habari atawakuta wanawake na wanamume ambao pia kama yeye wakio jikuta bila kupendelea wakiwa uwamishoni, na
ambao huendelea kufikiria namna gani wataendelea kutoa mchango wao nchini kwao,atimae wakimbizi kama yeye wanao fikiria kuhusu maisha yao ya baadae: namna gani watapata mahali pa kuishi,namna gani wataajiriwa kazini na namna gani familia yake itamuwasilia? Pia
namna gani ataendelea kuifanya shuhuli yake ambayo ameizowea kwa miaka kadhaa? Maisha hayo yanayo wakutanisha kwa miezi kadhaa hao wandugu kutoka nchi mbalimbali kama vile Cuba, Birmania, Côte d'Ivoire, Biélorussia, Haïti, Cameroun na kadhalika... ndio husababisha wafikirie kuhusu maisha yao ya baadae.
Jengo la wandishi wa habari hutoa malazi kwa wandishi wa habari thalathini kwa mwaka mmoja chini ya udhamini wa vituo mbalimbaki vya habari, na muungano wa nchi za Ulaya kwa wakimbizi: kwa kutoa kwa kila mwandishi wa habari chumba chake, kadi ya kujipatia Chakula, kadi ya mawasiliano na pia kadi ya uchukuzi na kuendelea kuwashirikisha kwa hiyari ya mtu kuifanya mazoezi ya shuhuli yake ya utangazaji kupitia uandishi wa habari ama utangazaji kwa masilahi ya jengo hilo la wandishi wa habari ambalo ndilo jicho la wanahabari wakimbizi.
|
 |
 |
 |
|
|
Contact
Maison des journalistes
35, rue Cauchy
75015 PARIS
Gari chini ya chini : Lourmel (ligne 8)
RER : Javel (ligne C)
Autobus : n°42, 70 ou 88
tel / fax :
00 33 140 60 04 02
|
 |
 |
 |